• HABARI MPYA

  Jumatatu, Desemba 24, 2018

  UGANDA YAWANIA NAFASI MBILI MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO

  UGANDA itakuwa na timu mbili katika mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
  Hizo ni Vipers iliyoporomoka kutoka Ligi ya Mabingwa baada ya kutolewa na CS Constantine ya Algeria na KCCA iliyofuzu kutoka Kombe la Shirikisho baada ya Mtibwa Sugar ya Tanzania.
  KCCA imefuzu kwa ushindi wa jumla wa 5-1, ikishinda 3-0 nyumbani na 2-1 ugenini, wakati Vipers imetolewa kwa jumla ya mabao 3-0 ikifungwa 1-0 ugenini na 2-0 nyumbani.
  Timu nyingine zilizoangukia hatua hii kutoka Ligi ya Mabingwa ni ZESCO United, Nkana FC za Zambia, Al-Hilal ya Sudan, Coton Sport ya Cameroon, Gor Mahia ya Kenya, Stade Malien ya Mali, Al-Ahly Benghazi, Al-Nasr za Libya, AS Otoho ya DRC, Jimma Aba Jifar ya Ethiopia, Bantu ya Lesotho, Ittihad Tanger ya Morocco, African Stars ya Namibia na ASC Diaraf ya Senegal.

  Timu nyingine zilizofuzu kutoka Kombe la Shirikisho ni Zamalek ya Misri, Raja Casablanca na RS Berkane, Hassania Agadir za Morocco, CS Sfaxien ya Tunisia, Hussein Dey ya Algeria, Petro de Luanda ya Angola, Salitas ya Burkina Faso, New Star ya Cameroon, Asante Kotoko ya Ghana, FC San Pedro ya Ivory Coast, Enugu Rangers ya Nigeria, Mukura Victory ya Rwanda na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.
  Upangwaji wa ratiba za mechi ya mechi za hatua hiyo utafanyika Ijumaa wiki hii, makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mjini Cairo nchini Misri, timu zilizofuzu kutoka Kombe la Shirikisho zikimenyana na timu zilizotolewa kwenye Ligi ya Mabingwa.  
  Na baada ya mechi hizo, washindi 15 watakwenda kuunga na Etoile du Sahel kukamilisha timu 16 za kucheza hatua ya makundi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: UGANDA YAWANIA NAFASI MBILI MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top