• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 22, 2018

  SOLSKJAER AANZA VYEMA MAN UNITED, WASHINDA 5-1 UGENINI

  Kiungo wa Manchester United, Jesse Lingard akishangilia baada ya kufunga mabao mawili dakika za 57 kwa penalti na 90 katika ushindi wa 5-1 dhidi ya wenyeji, Cardiff City leo kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Cardiff City.
  Mabao mengine ya Man United iliyocheza kwa mara ya kwanza chini ya kocha mpya wa muda, Mnorway Ole Gunnar Solskjaer baada ya kufukuzwa kwa Mreno, Jose Mourinho yamefungwa na Marcus Rashford dakika ya tatu, Ander Herrera dakika ya 29 na Anthony Martial dakika ya 41, wakati la Cardiff limefungwa na Victor Camarasa kwa penalti dakika ya 38. 
  Kwa ushindi huo, Manchester United inafikisha pointi 29 baada ya kucheza mechi 18, ikipanda kutoka nafasi ya nane hadi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England ikiwa inazidiwa pointi nane na Arsenal iliyo nafasi ya tano 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SOLSKJAER AANZA VYEMA MAN UNITED, WASHINDA 5-1 UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top