KLABU ya Marseille ya Ufaransa imemvunjia mkataba beki wake, Patrice Evra kufuatia mchezaji huyo kufungiwa miezi saba na Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA).
Beki huyo wa zamani wa Manchester United alimpiga teke shabiki wa klabu hiyo kabla ya mechi ya Europa League dhidi ya Vitoria wiki iliyopita.
Mara tu baada ya tukio hilo, klabu hiyo ya Ufaransa ilimsimamisha mchezaji huyo ili uchunguzi ufanyike na sasa wamethibitisha hatua hiyo baada ya kujiridhisha mchezaji huyo alifanya kitendo cha aibu.
0 comments:
Post a Comment