MSHAMBULIAJI Zlatan Ibrahimovic atarejea mapema kuliko ilivyotarajiwa kwenye kikosi cha Manchester United kikimenyana na Newcastle United kesho.
Kocha Mreno wa Man United, Jose Mourinho amesema kwamba pamoja na Ibrahimovic, anatarajia wachezaji wengine waliokuwa majeruhi, Paul Pogba na Marcos Rojo watarejea pia.
Mshambuliaji huyo wa Sweden, hajacheza kwa miezi saba tangu aumie mguu wake wa kulia katika goti kwenye mechi ya Europa League dhidi ya Anderlecht na alitarajiwa kuwa nje hadi mapema Desemba.
Pamoja na hayo, baada ya siku tatu za kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza viwanja vya Carrington, Mourinho amesema Ibrahimovic atarejea na ataanzia benchi kwenye mechi dhidi ya Newcastle.
Zlatan Ibrahimovic anatarajiwa kuanzia benchi kesho katika mechi dhidi ya Newcastle United PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Kikosi cha Mreno huyo kinazidiwa pointi nane na mahasimu, Manchester City baada ya kufungwa 1-0 na Chelsea mwanzoni mwa mwezi Uwanja wa Stamford Bridge, London kabla ya mapaumziko ya kupisha mechi za kimataifa.
0 comments:
Post a Comment