• HABARI MPYA

    Tuesday, November 03, 2015

    SAMATTA, YAYA WAINGIA 10 BORA YA MWANASOKA BORA AFRIKA 2015

    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ameingia kwenye orodha ya wachezaji 10 wanaowania Tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika mwaka 2015.
    Katika orodha iliyotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) jana, Samatta ni kati ya wachezaji watatu TP Mazembe walioingia 10 Bora, wengine wakiwa ni kipa Robert Kidiaba Muteba wa DRC na kiungo Roger Assale wa Ivory Coast.
    Mbwana Samatta kulia ameingia 10 bora ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika

    Watatu hao wanachuana na Abdeladim Khadrouf wa Morocco na Moghreb Tetouan, Baghdad Bounedjah wa Algeria na Etoile du Sahel, Felipe Ovono wa Equatorial Guinea na Orlando Pirates, Kermit Erasmus wa Afrika Kusini na Orlando Pirates, Mohamed Meftah wa Algeria na USM Alger, Mudather Eltaib Ibrahim ‘Karika’ wa Sudan na El Hilal na Zineddine Ferhat wa Algeria na USM Alger.
    Katika orodha ya wachezaji wa 10 wanaowania tuzo ya jumla ya Mwanasoka Bora wa Afrika, Yaya Toure wa Ivory Coast na Manchester City ataitetea tuzo hiyo dhidi ya Andre Ayew wa Ghana na Swansea, Aymen Abdennour wa Tunisia na Valencia na Mudather Eltaib Ibrahim ‘Karika’ wa Sudan na El Hilal.
    Wengine ni Mohamed Salah wa Misri na Roma, Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon na Borussia Dortmund, Sadio Mane wa Senegal na Southampton, Serge Aurier wa Ivory Coast na Paris Saint Germain, Sofiane Feghouli wa Algeria na Valencia na Yacine Brahimi wa Algeria na Porto.
    Washindi watatokana na kura za makocha wa timu za taifa barani na Wakurugenzi wa Ufundi wa Vyama vya Soka vya nchi wanachama wa CAF.
    Sherehe za tuzo zinatarajiwa kufanyika Alhamisi ya Januari 7 mwaka 2016 mjini Abuja, Nigeria.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA, YAYA WAINGIA 10 BORA YA MWANASOKA BORA AFRIKA 2015 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top