Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Nteze John Lungu amesema kwamba ana imani na makocha wa sasa wa timu ya taifa, Charles Boniface Mkwasa na Mshauri wake wa Ufundi, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ wanaweza kuipa matokeo mazuri timu.
Akitoa maoni yake kuelekea mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Algeria katikati ya mwezi huu, Nteze amesema anawafahamu Kibadeni na Mkwasa ni makocha wazuri kwa kuwa wote wamemfundisha.
“Sina cha kusema zaidi ya kuwatakia kila la kheri waweze kushinda mechi hiyo na nyingine zijazo. Makocha wote wamenifundisha na wana uwezo mkubwa sana. Tunasubiri ushindi,”amesema Nteze akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE kwa simu jana kutoka mjini Bellevue, Washington, Marekani.
Kuhusu Algeria, Nteze amesema kwamba ni timu nzuri na bora kwa sasa Afrika, lakini haimaanishi kwamba haiwezi kufungwa na Tanzania. “Algeria ni timu nzuri sana, wakati wangu nakumbuka tulicheza nao kwao walitufunga nasi tuliwafunga nyumbani,”amesema.
Taifa Stars ilikutana na Algeria mwaka 1995 katika mechi za kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika zilizofanyika Afrika Kusini mwaka 1996 na kila timu ilishinda 2-1 nyumbani kwake.
Mchezo wa Dar es Salaam, Algeria walianza kupata bao la mapema baada ya beki Mustafa Hoza kumrudishia mpira kipa Steven Nemes ambaye alipojaribu kumpiga chenga mchezaji wa Algeria, akaunasa na kufunga.
Taifa Stars ikasawazisha kipindi hicho hicho cha kwanza kwa bao la Juma Bakari ‘Kidishi’ aliyepokea pasi ya Sekilojo Chambua kabla ya Madaraka Suleiman kumalizia kona ya Nteze kipindi cha pili kuifungia Tanzania bao la ushindi. Na bao la Stars mjini Algiers lilifungwa na Mohammed Hussein ‘Mmachinga’.
Novemba 14 na 17 Taifa Stars na Algeria zitakutana katika mechi mbili za mtoano kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 Urusi, Tanzania wakianzia nyumbani.
Tanzania ambayo imefika hatua hii baada ya kuitoa Malawi kwa jumla ya mabao 2-1, ikishinda 2-0 nyumbani na kufungwa 1-0 Blantyre, imeweka kambi Afrika Kusini tangu jana kujiandaa na mchezo huo.

![]() |
Nteze John (katikati) akiwa na mabinti zake,Regina (kulia) na Venis (kushoto) |

0 comments:
Post a Comment