• HABARI MPYA

    Sunday, October 11, 2015

    CHAD YAIPIGA 1-0 SIERRA LEONE KUFUZU KOMBE LA DUNIA

    TIMU ya Chad imeifunga bao 1-0 Sierra Leone jana katika mchezo wa kwanza wa mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 Urusi.
    Shukrani kwake, winga Leger Djimrangar aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 47 na kuwapa furaha Wachad mjini N'Djamena.
    Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) iliyolazimika kucheza mechi ya nyumbani na Madagascar mjini Antananarivo kwa sababu ya vurugu mjini Bangui, imepata kipigo kilichotarajiwa cha mabao 3-0.
    Chad imeshinda 1-0 jana dhidi ya Sierra Leone

    Eritrea imerudi na mguu mbaya katika soka ya kimataifa baada ya kuchapwa maabo 2-0 nyumbani na Botswana.
    Kutakuwa na mechi tatu za marudiano leo na nyingine 10 Jumanne na washindi wa jumla wataungana na timu nyingine 27 kwa mechi za mwisho za mchujo Novemba.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHAD YAIPIGA 1-0 SIERRA LEONE KUFUZU KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top