REAL Madrid imefanya kufuru La Liga, baada ya kuifunga mabao 9-1 Granada mchana wa leo, huku Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo peke yake akifunga mabao matano.
Ronaldo alitumia dakika nane kufunga hat-trick kipindi cha kwanza katika dakika za 31 36 na 38 na sasa amemfikia Lionel Messi wa Barcelona kwa kufunga hat-tricks 24 kila mmoja La Liga. Nyota huyo wa Ureno aliongeza mabao mawili zaidi katika dakika za 54 na 89.
Karim Benzema pia alifunga mabao mawili katika dakika za 52 na 56, wakati mabao mengine Gareth Bale alifunga moja, lililokuwa la kwanza Uwanja wa Santiago Bernabeu.
Diego Mainz Garcia alijifunga kuipatia bao linguine Real dakika ya 83, wakati bao la kufutia machozi la Granada lilifungwa na Roberto Ibanez dakika ya 74.
Kikosi cha Carlo Ancelotti sasa kinazidiwa pointi moja tu na vinara Barcelona katika msimamo wa La Liga, 68-67 ingawa Real wamecheza mechi moja zaidi (28-29). Barca watakuwa wageni wa Celta Vigo usiku wa leo.
Kikosi cha Real Madrid kilikuwa; Casillas, Arbeloa, Ramos, Varane, Marcelo, Rodriguez/Jese dk61 Kroos/Illaramendi dk57, Modric, Bale, Benzema/Hernandez dk61 na Ronaldo.
Granada: Oier, Foulquier, Mainz, Babin/Murillo dk61, Juan Carlos, Fran Rico/Silvestre dk57, Iturra, Ibanez, Rochina/Piti dk53, Candeias na El Arabi.
Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia mabao matano Real Madrid katika ushindi wa 9-1 leo
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3026335/Real-Madrid-9-1-Granada-Cristiano-Ronaldo-nets-FIVE-Karim-Benzema-Gareth-Bale-score.html#ixzz3WRD18ghi


.png)
0 comments:
Post a Comment