• HABARI MPYA

  Saturday, December 20, 2014

  TFF YATAKA MGOGORO ZFA UMALIZWE

  KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imeagiza pande mbili zinazosigana ndani ya Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) kumaliza tofauti zao.
  Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kitendo hicho ni kinyume cha taratibu za uendeshaji mpira wa miguu ambazo zinakataza masuala ya mchezo huo kupelekwa katika mahakama za kawaida.
  TFF imetoa rai kwa pande zote mbili zinazohusika na mgogoro huo kukaa kwenye meza ya mazungumzo ili kumaliza tofauti zao.
  Rais wa TFF, Jamal Malinzi

  TFF imesema imejitolea kutuma ujumbe wake Zanzibar ili ukutane na pande zinazohusika katika mgogoro huo.
  “Ni muhimu usuluhisho upatikane haraka ili tuweze kujua hatma ya washiriki wetu kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi,”imesema taarifa ya TFF.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF YATAKA MGOGORO ZFA UMALIZWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top