• HABARI MPYA

  Thursday, January 01, 2015

  HERI YA MWAKA MPYA 2015

  BODI ya Ukurugenzi, Menejimenti na wafanyakazi wote wa BIN ZUBEIRY Blog inawatakia heri ya mwaka mpya wasomaji wake wote. Wakati tunaingia katika mwaka wa tatu tangu kuanza kwetu kutoa huduma hii, pamoja na kutoa shukrani za dhati kwa wadau, taasisi na watu mbalimbali wakiwemo wasomaji wetu kwa kuwa nasi ziku zote hizo, pia tunawaahidi kuendeleza ufanisi katika kazi.
  Tunachukua fursa hii, kuwaomba radhi pale tulipojikwaa na kwa namna moja au nyingine tukawakwaza. Dhamira yetu ni kuwafanya mfurahie chombo chenu, na inapotokea tofauti, basi dhahiri hiyo inakuwa ni bahati mbaya.

  Kuelekea mwaka 2015, tumejipanga kuhakikisha tunaongeza umakini na ufanisi zaidi, ili kuendelea kuwafurahisha wasomaji wetu. Tunatambua, changamoto ni nyingi, lakini tumejipanga kuendelea kukabiliana nazo, ili mradi tu BIN ZUBEIRY iendelee kuwa chombo kinachoheshimika, kuaminika na kukubalika. Kusimamia kwenye misingi, miiko na maadili ya taaluma ya Habari- hiyo inabaki kuwa dhamira yetu kuu kuelekea mwaka 2015. Kwa mara nyingine tena, tunawashukuru wale wote ambao kwa namna moja au nyingine ni wadau wa blogu yetu. Tunawatakia heri ya mwaka mpya 2015. Mungu awajaalie uwe mwaka mwingine wenye mafanikio kwenu. Amin. Heri ya Mwaka Mpya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HERI YA MWAKA MPYA 2015 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top