• HABARI MPYA

  Saturday, December 13, 2014

  KIIZA ATUA SIMBA SC, BARUA YAMKWAMISHA KUCHEZA NANI MTANI JEMBE LEO

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  HAMISI Kiiza ‘Diego’ yuko mbioni kujiunga na Simba SC na anachosubiri ni kupewa barua tu ya kuachwa na Yanga SC.
  Mganda huyo aliondoka kambini Yanga SC juzi kufuatia klabu hiyo kumsajili Mliberia, Kpah Sean Sherman.
  “Kama Yanga watampa barua ya kumuacha, hata leo sisi tunamtumia,”amesema kiongozi mmoja wa Simba SC (jina tunalihifadhi) akizungumza na BIN ZUBEIRY leo.
  Simba na Yanga SC zinamenyana jioni hii katika mechi ya Nani Mtani Jembe Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na iwapo Kiiza atacheza leo, kwa kuwa hajapewa barua ya kuachwa inaweza kumgharimu.
  Hamisi Kiiza kulia amejiunga na Yanga SC

  Anaweza kupoteza haki zake ambazo Yanga SC wanatakiwa kumlipa baada ya kuvunja naye Mkataba pia- kwa klabu hiyo kumgeuzia kibao kwamba yeye ndiye amevunja Mkataba.   
  Kiiza ameondoka bila ya kufukuzwa, lakini baada ya kusikia taarifa za ‘juu juu’ kwamba akisajiliwa Sherman, yeye ataachwa.
  Habari zaidi zinasema, Kiiza tayari amejiunga na Simba SC, lakini anasubiri kupewa barua ya kuachwa, ili aanze maisha mapya Simba SC.
  Kiiza alijiunga na Yanga SC mwaka 2011 akitokea Bunamwaya ya Uganda na kwa kipindi cha chote amekuwa mmoja wa wafungaji tegemeo wa timu hiyo.     
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIIZA ATUA SIMBA SC, BARUA YAMKWAMISHA KUCHEZA NANI MTANI JEMBE LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top