• HABARI MPYA

  Friday, December 19, 2014

  JERRY MURO ALIVYOANZA KAZI JANGWANI LEO...

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  JERRY Muro, amesema yeye si Msemaji wa Yanga SC, bali ni Mkuu w2a Idara ya Habari na Mwasiliano ya klabu.
  Muro, Mtangazaji wa zamani wa ITV na TBC amesema hayo leo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kwa mara ya kwanza kama mtumishi wa klabu hiyo, makao makuu, Jangwani, Dar es Salaam. 
  Muro leo alitoa taarifa ya mabadiliko ya benchi la ufundi na Sekretarieti ya klabu hiyo kongwe hiyo  kwa niaba ya Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Manji.
  Amesema Mholanzi Hans van der Pluijm ambaye miezi 12 anachukua nafasi ya Marcio Maximo huku mzalendo Charles Boniface Mkwasa 'Master' anachukua nafasi ya Leonardo Leiva.
  Jerry Muro makao makuu ya klabu ya Yanga SC leo alipozungumza kwa mara ya kwanza

  "Mwenyekiti wa Yanga anapenda kuchukua fursa hii kuwashukuru Marcio Maximo pamoja na msaidizi wake Neiva kwa ushirikiano wao katika kufundisha timu ya Yanga kwa muda wa miezi sita iliyopita na anawatakia kila la kheri katika safari yao na Mungu akipenda wataendelea kushirikiana nasi katika siku za mbele,”amesema  Muro.
  Aidha mbali na mabadiliko hayo pia Yanga imetangaza rasmi sekretarieti mpya ya klabu hiyo kufuatia waliokuwepo kutoongezeqwa mikataba yao ambapo sasa Katibu Mkuu atakuwa Dk Jonas Tiboroha huku Mkuu wa Idara ya Masoko akiwa Omar Kaya.
  Mbali na hao pia wapya walioingia kuongoza klabu hiyo ni pamoja na Muro anayekuwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano,Frank Chacha akiwa Mkuu wa Idara ya Sheria wakati Baraka Deusdedit akiwa Mkuu wa Idara ya Fedha.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JERRY MURO ALIVYOANZA KAZI JANGWANI LEO... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top