• HABARI MPYA

  Saturday, December 20, 2014

  GOR MAHIA, AFC LEOPARDS ZAHAMIA RWANDA KUSAKA WACHEZAJI

  Na Vincent Malouda, NAIROBI
  VIGOGO wa ligi kuu ya taifa la Kenya, Gor Mahia na AFC Leopards sasa wamekita mizizi yao nchini Rwanda kuwatafuta wachezaji wa kuwasajili wakati wa dirisha refu la usajili wa wachezaji nchini Kenya.
  Klabu ya Gor Mahia imo mbioni kuwasajili wachezaji wa Rayon Sports na mabeki Abouba Sibomana na Karim Nizigiyimana.
  Sibomana, 25, alithibitisha kuwa amefanya mazungumzo na K’Ogalo na yupo tayari kujiunga nao iwapo wataununua mkataba wake wa miezi sita na Rayon Sports.
  Gor Mahia imehamishia mawindo ya wachezaji Rwanda, baada ya nyota wake wengi kutimka msimu huu

  “Tushaelewana kila kitu. Kilichobaki ni wao (Gor Mahia) kuafikiana na klabu yangu ya Rayon Sport,” Sibomana aliliambia gazeti la Rwanda la New Times.
  Leopards na Gor pia wanawinda sahihi ya wing’a wa APR Charles Tibingana.  Dirisha refu la uhamisho nchini Kenya lilifunguliwa tarehe mosi Desemba na litafungwa tarehe 31 Januari mwaka 2015.
  Tayari Gor ambao ni mabingwa wa 2014 wamewapoteza wachezaji Dan Sserunkuma na Geoffrey ‘Baba’ Kizito waliyoelekea Simba SC na Vietnam mtawalia.
  Mabwenyenye hao vile vile wanawania sahihi ya straika la URA ya Uganda Robert Ssentongo na aliyekuwa mshambulizi wa Yanga Brian Umony.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GOR MAHIA, AFC LEOPARDS ZAHAMIA RWANDA KUSAKA WACHEZAJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top