• HABARI MPYA

    Sunday, April 13, 2014

    REAL MADRID YAREJEA KILELENI LA LIGA

    REAL Madrid imehitimisha wiki nzuri kwa kurudi kileleni mwa La Liga, baada ya usiku wa jana kuitandika Almeria mabao 4-0, ikitoka kutinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
    Ikicheza bila mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo, Real ilipata mabao yake kupitia kwa Angel Di Maria dakika ya 28, Gareth Bale dakika ya 53, Isco dakika ya 56 na Morata dakika ya 85.
    Raha tupu; Gareth Bale ameifungia Real jana ikirejea kileleni mwa La Liga

    Real sasa inatimiza pointi 79 za mechi 33 na kupaa kileleni kwa wastani wa mabao kwa kuwa na pointi sawa na Atletico Madrid, ikiizidi kwa pointi moja Barcelona. Lakini Real wanaweza kushuka hadi nafasi ya pili leo iwapo Atletico Madrid itaifunga Getafe.
    Katikati ya wiki, Real imeitoa Borussia Dortmund katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na kutinga Robo Fainali, ambako itakutana na mabingwa watetezi, Bayern Munich.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: REAL MADRID YAREJEA KILELENI LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top