• HABARI MPYA

  Jumapili, Aprili 27, 2014

  CHELSEA YAIPIGA 2-0 LIVERPOOL ANFIELD,VITA YA UBINGWA ENGLAND INOGILE

  CHELSEA imeifunga Liverpool mabao 2-0 Uwanja wa Anfield katika mchezo wa Ligi Kuu ya England na kufufua matumaini ya ubingwa.
  Mabao ya Chelsea inayofundishwa na Mreno Jose Mourinho yamefungwa na Demba Ba dakika ya 45 na ushei Willian aliyemalizia kazi nzuri ya Fernando Torres dakika ya 90 na ushei.
  Chelsea sasa inatimiza pointi 78 baada ya kucheza mechi 36 sawa na Liverpool inayoongoza kwa pointi zake 80, wakati Manchester City yenye pointi 74 za mechiu 34 ni ya tatu.
  Raha tupu: John Obi Mikel akishangilia mbele ya kundi la wenzake wanaompongeza Demba Ba kwa kufunga bao la kwanza
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHELSEA YAIPIGA 2-0 LIVERPOOL ANFIELD,VITA YA UBINGWA ENGLAND INOGILE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top