• HABARI MPYA

  Jumatano, Aprili 30, 2014

  KATIBU MKUU WA FIFA AWASILI KESHO DAR

  KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Soka la Kimataifa  (FIFA), Jerome Valcke anawasili nchini kesho (Mei 1 mwaka huu) ambapo atafungua semina ya mawasiliano kwa nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

  Valcke ambaye atafuatana na maofisa wengine saba wa FIFA baadaye kesho hiyo hiyo (Mei 1 mwaka huu) atakuwa na mkutano na waandishi wa habari. Mkutano huo utafanyika saa 4 kamili asubuhi kwenye hoteli ya Double Tree by Hilton iliyopo Oysterbay, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KATIBU MKUU WA FIFA AWASILI KESHO DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top