• HABARI MPYA

  Jumanne, Aprili 22, 2014

  GIGGS KOCHA MPYA MAN UNITED BAADA YA MOYES KUTUPIWA VIRAGO 'KINYAMA'

  HATIMAYE kocha David Moyes amefukuzwa Manchester United baada ya miezi 10 na sasa Ryan Giggs atakaimu nafasi yake wakati mchakato wa kusaka kocha mpya ukiendelea.
  Mtendaji Mkuu, Ed Woodward aliwasili Carrington majira ya Saa 2:00 asubuhi leo kumueleza kocha huyo Mscotland uso kwa uso habari za kufukuzwa kwake.
  Moyes aliushukuru uongozi wa klabu baada ya mazoezi juu ya kuondka kwake. Wachezaji hawakuwapo wakati huo. 
  Taarifa katika akaunti ya Twitter ya klabu imesema: 'BREAKING: Manchester United inatangaza kwamba David Moyes ameondoka klabuni. Klabu inapenda kumshukuru kwa kazi ngumu, ukweli na weledo alioleta kwenye timu.
  Ryan Giggs atakuwa kocha wa muda kumalizia msimu. 
  Iligundulika jana familia ya Glazer ambao ni wamiliki wa United, ilipoteza imani na Moyes baada ya timu hiyo kuboronga kwenye Ligi Kuu England na kuangukia nafasi ya saba kwenye msimamo.
  Kipigo cha mwisho cha mabao 2-0 Jumapili kutoka kwa Everton, ambacho ni cha 11 katika Ligi Kuu msimu huu na kinawafanya mabingwa hao watetezi wazidiwe pointi 13 kwenye nafasi za ubingwa- ndio kimehitimisha safari yake.

  Sema kwaheri: Wamiliki wa United, familia ya Glazer imemfukuza Moyes baada ya matokeo mabaya
  Confirmation: Manchester United released a short statement on Twitter
  Uthibitisho: Taarifa ya Manchester United kwenye Twitter
  Arrival: Ryan Giggs, who will take temporary charge until the end of the season, arrives at Carrington on Tuesday morning
  Anawasili: Ryan Giggs, ambaye atakuwa kaimu kocha mkuu hadi mwishoni mwa msimu, akiwasili makao makuu ya klabu Carrington leo
  Early morning meeting: United executive vice-chairman Ed Woodward delivered the news face-to-face on Tuesday morning
  Mapema asubuhi ya leo Makamu Mwenyekiti, Ed Woodward alimpelekea taarifa Moyes uso kwa uso juu ya kufukuzwa kwake

  DAVID MOYES MAN UNITED

  Amecheza mechi 51
  Ameshinda mechi 27
  Ametoa sare mechi 9
  Amefungwa mechi 15
  Asilimia ya ushindi ni 52.94
  Kichapo cha juzi cha mabao 2-0 kutoka kwa Everton ndicho kilihitimisha maisha ya Moyes United kwa sababu kilimaanisha timu hiyo ilikuwa imepoteza mechi yake ya 11 msimu huu na wako nyuma kwa pointi 13 kutoka katika nafasi ya nne.
  Familia ya Glazer na Mtendaji Mkuu wa United, Ed Woodward walikuwa wamepania kumvumilia Moyes, lakini wameona kiwango cha timu yao kinazidi kuporomoka kila wiki na wachezaji wanaonekana kuacha kujitoa kwa ajili ya kocha wao.
  Makocha Jurgen Klopp wa Borussia Dortmund, Louis van Gaal wa Uholanzi na Carlo Ancelotti wa Real Madrid wanatajwa kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuchukua ukocha wa kudumu mwishoni mwa msimu.
  Licha ya usajili wa fedha nyingi kwa Marouane Fellaini wakati wa kiangazi na Juan Mata, Januari, United imeshindwa kupambana na wapinzani wao kwenye mbio za ubingwa.
  Moyes ambaye alirithi mikoba ya Sir Alex Ferguson wakati wa kiangazi, pia amechemka kwenye michuano mingine msimu huu, United ilitolewa na Swansea City katika hatua ya tatu ya Kombe la FA, wakati Sunderland waliwatoa kwenye nusu fainali ya Kombe la Ligi na Bayern Munich kwenye Ligi ya Mabingwa.
  Katika michuano yote Moyes kashinda mechi 27 kati ya 51 akitoka sare mara nane na kufungwa mara 15.

  MECHI ZILIZOBAKI

  Aprili 26 Norwich City (nyumbani)
  Mei 3 Sunderland (nyumbzani)
  Mei 6 Hull City (nyumbani)
  Mei 11 Southampton (ugenini)
  Katika hatua nyingine uongozi wa Manchester United chini ya Familia ya Glazer na Ed Woodward, tayari una majina matatu ya makocha wakubwa  ambao wamekuwa na mafanikio makubwa msimu huu, ambapo jina la kwanza na ambalo linapigiwa chapuo kubwa ni la Jurgen Klopp ambapo uongozi wa Man umekubali kulipa fedha kwa ajili ya kuvunja mkataba wake mrefu na Borussia Dortmund .
  Kocha mwingine Laurant Blanc ambaye amewahi kucheza United na kwa ni kocha Paris Saint-Germain, -(PSG) mabingwa wapya wa Ufaransa. Hata hivyo uongozi wa United umekiri kuwepo kwa ugumu wa kumpata Blanc kutokana na mkataba wake, ingawa wanaamini anaweza kuvutiwa na uzalendo wake kwa timu hiyo ya Old Trafford.
  Diego Simeone anayetamba hivi sasa na Atletico Madrid, naye yumo katika orodha hiyo ya kuchukua nafasi ya Moyes, na uongozi huo umesema hawatakuwa na pingamizi lolote kuvunja benki kwa ajili ya kumpata mtu sahihi kwa mafanikio ya United.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: GIGGS KOCHA MPYA MAN UNITED BAADA YA MOYES KUTUPIWA VIRAGO 'KINYAMA' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top