• HABARI MPYA

  Jumatano, Aprili 30, 2014

  BREAKING NEWS; FRANK DOMAYO NAYE AANGUKA MIAKA MIWILI AZAM FC, JANGWANI WATAOMBA POO MWAKA HUU

  Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
  KIUNGO mkabaji wa Yanga SC, Frank Domayo amesaini Mkataba wa miaka miwili kujiunga na mabingwa wapya wa Tanzania Bara, Azam FC jioni ya leo mjini Mbeya.
  Domayo amesaini Azam FC baada ya kumaliza Mkataba wake wa miaka miwili na Yanga SC, ambayo alijiunga nayo akitokea JKT Ruvu miaka miwi iliyopita.
  Katibu wa Azam FC, Nassor Idrisa Mohamed ‘Father’ amesema katika kuendelea kukiimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao wamepiga hatua nyingine kwa kumsaini Domayo.
  Kutoka Jangwani hadi Chamazi; Frank Domayo akisaini Mkataba wa Azam FC leo
  Frank Domayo akitia dole gumba, maana yake ni mchezaji mpya wa Azam FC 

  “Kama unavyojua, baada ya kumaliza msimu vizuri tukiwa mabingwa wa Bara, tuligundua mapungufu kwenye kikosi chetu na kwa ushauri wa mwalimu wetu (Joseph Marius Omog) ndiyo tunayafanyia kazi,”alisema Father.
  Domayo anakuwa mchezaji wa wa pili ndani ya siku mbili kusajiliwa na Azam FC kutoka mabingwa wa zamani na mabingwa wa kihistoria Tanzania Bara, Yanga SC baada ya jana klabu hiyo kumsaini mshambuliaji Mrundi Didier Kavumbangu.    
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BREAKING NEWS; FRANK DOMAYO NAYE AANGUKA MIAKA MIWILI AZAM FC, JANGWANI WATAOMBA POO MWAKA HUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top