• HABARI MPYA

  Jumamosi, Aprili 26, 2014

  KABUMBANGU: YANGA SC WAMENICHUNIA, MKATABA UMEISHA

  Na Renatus Mahima, Dar es Salaam
  DIDIER Kavumbagu, nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Burundi (Intamba Mu Rugamba), amesema yuko sokoni baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY muda mfupi uliopita, Kavumbagu ambaye alikuwa kinara wa upachikaji mabao kwa Yanga msimu wa 2012/13 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, amesema mkataba wake na timu hiyo ya Jangwani umemalizika na sasa ni mchezaji huru.
  "Nimemaliza mkataba wangu na Yanga, nimewasubiri sana lakini mpaka sasa hakuna hata kiongozi mmoja wa klabu hiyo aliyenifuata kwa ajili ya mazungumzo ya kuongeza makataba.
  Didier Kavumbangu amesema Yanga SC wamemchunia

  "Baada ya kumaliza mkataba, niliipa kipaumbele Yanga kwa sababu wao ndio walinileta Tanzania lakini sasa ninaona wako kimya. Ligi Kuu ya Tanzania iko mgumu na ninapenda niendelee kucheza hapa," amesema zaidi Kavumbagu.
  Beno Njovu, Katibu Mkuu wa Yanga, alipotafutwa na BIN ZUBEIRY kuzungumzia suala hilo, amesema: "Kwa sasa niko nje ya ofisi na huu si muda mwafaka wa kuzungumzia masuala ya usajili. 
  Katika misimu miwili ya kuichezea klabu hiyo, Kavumbangu amefunga mabao 31 katika mechi 63 za mashindano yote, moja tu la penalti. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KABUMBANGU: YANGA SC WAMENICHUNIA, MKATABA UMEISHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top