• HABARI MPYA

    Tuesday, April 29, 2014

    AL AHLY YAPANGWA KUNDI LA ‘KIFO’ KOMBE LA SHRIKISHO, KUNA ETOILE NA SEWE SPORT YA IVORY COAST

    Na Princess Asia, Dar es Salaam
    VIGOGO wa Misri, Al Ahly wamepangwa katika Kundi B la Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2014 pamoja na Sewe Sport ya Ivory Coast, Etoile du Sahel ya Tunisia na Nkana FC ya Zambia.
    Katika droo iliyopangwa leo makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), wababe wa Cameroon, Coton Sport wametupwa Kundi A pamoja na ASEC Mimosas ya Ivory Coast, AS Real ya Mali na AC Leopards ya Kongo Brazzaville.
    Kundi la kifo; Al Ahly imepangwa kundi gumu Kombe la Shirikisho Afrika 


    Mechi zinatarajiwa kuchezwa kuanzia kati ya Mei 16 na 18 na Juni 23 na 25, Juni 6 na 8, Julai 25 na 27, Agosti 8 na 10 na 22-24 na washindi wawili wa kila kundi watasonga Nusu Fainali.MAKUNDI KOMBE LA SSHIRIKISHO:
    KUNDI A: AC Leopards, ASEC Mimosas, AS Real Bamako na Coton Sport
    KUNDI B: Al Ahly, Etoile du Sahel, Sewe San Pedro na Nkana FC
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AL AHLY YAPANGWA KUNDI LA ‘KIFO’ KOMBE LA SHRIKISHO, KUNA ETOILE NA SEWE SPORT YA IVORY COAST Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top