• HABARI MPYA

  Jumapili, Aprili 20, 2014

  SIMBA NA YANGA KATIKA PICHA JANA TAIFA

  Mshambuliaji wa Yanga SC, Hamisi Kiiza akimiliki mpira mbele ya wachezaji wa Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
  Wachezaji wa Simba SC wakimpongeza mfungaji wa bao lao la kuongoza, Haroun Chanongo aliyevua jezi huku akifuta machozi ya kilio cha furaha
  Mfungaji wa bao la kusawazisha la Yanga SC, Simon Msuva kushoto akishangilia na wenzake
  Beki wa Simba SC, Mganda Joseph Owino kushoto akipiga kichwa dhidi ya mshambuliaji wa Yanga SC, Didier Kavumbangu
  Kocha wa Simba SC, Mcroatia Zdravko Logarusic akitoa maelekezo kwa wachezaji wake
  Kocha wa Yanga SC, Mholanzi Hans van der Pluijm akiwatazama vijana wake
  Wachezaji wa Yanga SC baada ya kukabidhiwa Medali za ushindi wa pili Ligi Kuu iliyofikia tamati jana kwa Azam FC kutwaa ubingwa
  Simon Msuva akimtoka Amri Kiemba
  Hamisi Kiiza akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Simba SC, Nassor Masoud 'Chollo'
  Kikosi cha Yanga SC jana
  Kikosi cha Simba SC jana

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA NA YANGA KATIKA PICHA JANA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top