• HABARI MPYA

  Jumamosi, Aprili 26, 2014

  KATIBU WA TASWA APAA ULAYA

  Na Dina Ismail, Dar es Salaam
  CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinatarajia kushiriki kwenye Mkutano Mkuu wa 77 wa Chama cha Kimataifa cha Waandishi wa Habari za Michezo (AIPS) unaotarajiwa kuanza kesho (Jumapili) jijini Baku, Azerbaijan hadi Mei mosi mwaka huu.
  Taarifa ya TASWA, imesema kwamba Mkutano huo wa kawaida wa mwaka utashirikisha viongozi wa  vyama vya waandishi wa habari za michezo zaidi ya 150 duniani ambao ni wanachama wa AIPS na pia kutafanyika mikutano ya mabara ya vyama vya waandishi wa habari za michezo, ambao pia TASWA.
  Katibu wa TASWA, Amir Mhando kushoto akiwa na Mwenyekiti wake, Juma Pinto

  Pamoja na mambo mengine kutaendeshwa semina kuhusiana na masuala mbalimbali ya kuwaendeleza waandishi wa habari za michezo na pia utajadili changamoto zinazoikabili tasnia ya habari hasa wakati huu wa kukua kwa kasi kwa sayansi na teknolojia pamoja na mitandao ya kijamii.
  Katika mkutano huo, TASWA itawakilishwa na Katibu Mkuu, Amir Mhando ambaye anatarajiwa kuondoka leo (Jumamosi) jioni kwa ndege ya Qatar Airways akipitia Doha, Qatar.
  TASWA inamshukuru sana Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kwa kugharamia tiketi ya Katibu Mkuu kwenda na kurudi katika mkutano huo na hiyo inaonesha namna gani taasisi hizo mbili zinavyofanya kazi kwa kushirikiana.
  Chama chetu ni mwanachama hai wa AIPS yenye makao yake makuu Lausanne, Uswisi, ndiyo sababu kila mwaka tumekuwa tukishiriki mikutano ya namna hiyo, ambayo hushirikisha viongozi wa juu wa nchi wanachama.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KATIBU WA TASWA APAA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top