• HABARI MPYA

  Jumanne, Aprili 22, 2014

  GUARDIOLA AZUNGUMZIA KUHAMIA KWAKE MAN UNITED, ASEMA...

  KOCHA Pep Guardiola amekanusha tetesi za kuhamia Manchester United kutoka Bayern Munich anakopiga mzigo hivi sasa.
  David Moyes amefukuzwa leo United asubuhi na zikaibuka tetesi kwamba kocha huyo Mspanyola anapewa nafasi kubwa ya kurithi mikoba.
  Lakini Guardiola ameruka kimanga mapema, akizungumza na Waandishi wa Habari katika mkutano maalum kuelekea mchezo wa Nusu Fainali ya kwanza Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid.
  Hakuna kitu kama hicho: Pep Guardiola amesema anabaki Bayern Munich na kukanusha tetesi za kuhamia Manchester Untied
  Despair: David Moyes has been sacked by the club after less than a season in charge
  Amepigwa chini: David Moyes amefukuzwa baada ya karibu msimu mmoja wa kuwa kazini

  Alipoulizwa kama ana nia ya kuhamia United, Pep alisema: "Nipo hapa. Nipo Bayern na ninataka kubaki kwa miaka miwili zaidi kumalizia kazi yangu. Tumeshinda taji la Bundesliga, lakini nafikiri timu inaweza kufanya vizuri zaidi. 
  "Nafahamu vizuri kutoka staili ya ligi ya Hispania na kubadilisha kwenye staili ya Ujerumani haikuwa rahisi kwangu na ninahitaji muda zaidi ili kuhisi hii ni timu yangu haswa. 
  "Nahisi kweli Bayern ni timu yangu, lakini nafikiri tunaweza kucheza vizuri na kuimarika. Kwa maana hiyo nafikiri nina kazi ya kufanya na ndiyo maana ninataka kubaki zaidi hapa. Niko vizuri hapana watu wanaamini kazi yangu,"amesema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: GUARDIOLA AZUNGUMZIA KUHAMIA KWAKE MAN UNITED, ASEMA... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top