• HABARI MPYA

  Jumamosi, Aprili 19, 2014

  CHELSEA YAPIGWA 2-1 NA SUNDERLAND DARAJANI...MOURINHO UBINGWA SASA NDOTO

  CHELSEA imezidi kujitoa kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya kufungwa mabao 2-1 na Sunderland usiku huu Uwanja wa Stamford Bridge, London.
  Kipigo hicho kinaifanya The Blues ya Jose Mourinho ibaki na pointi zake 75 baada ya kucheza mechi 35 ikibaki nafasi ya pili, nyuma ya Liverpool inayoongoza kwa pointi zake 77 za mechi 34.
  Dogo anatisha; Connor Wickham akishangilia bao lake leo


  Mchezaji wa Chelsea, Cesar Azpilicueta akiwa amemuangukia kipa wa Sunderland, Vito Mannone

  Mkongwe Samuel Eto'o alianza kuifungia Chelsea dakika ya 12 akimalizia pasi ya Willian, lakini Sunderland ikatoka nyuma kwa mabao ya Connor Wickham dakika ya 18 na Fabio Borini dakika ya 82 kwa penalti kuibuka mshindi wa mechi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHELSEA YAPIGWA 2-1 NA SUNDERLAND DARAJANI...MOURINHO UBINGWA SASA NDOTO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top