• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 24, 2014

  VODACOM KUWAJAZA MABINGWA AZAM FC MILIONI 100 KASORO KIDOGO, TAMBWE KUPEWA MILIONI 5 NA UPUUZI

  Na Renatus Mahima, Dar es Salaam
  MSHAMBULIAJI Amisi Tambwe wa Simba atalamba Sh. milioni 5.2 za zawadi ya mfungaji bora zitakazotpolewa na wadhamini wakuun wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kampuni ya huduma ya simu ya Vodacom Tanzania baada ya kuibuka mfungaji bora wa msimu wa 2013/14 wa ligi hiyo.
  Aidha, timu yenye nidhamu italamba Sh. milioni 16 ikiwa ni ongezekon la Sh. milioni moja ikilinganishwa na ilivyokuwa msimu uliopita.
  Hayo yamebainishwa na Ofisa Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim katika mkutano na waandishi wa habari muda mfupi uliopita kwenye ofisi za Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) zilizopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
  Zawadi nono: Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa Vodacom,Salum Mwalimakizungumza katikati leo 

  ZAWADI ZA WASHINDI LIGI KUU BARA 2013/2014

  Bingwa: Sh. Milioni 75
  Mshindi wa Pili: Sh. Milioni 37
  Mshindi wa Tatu: Sh. Milioni 26

  Mshindi wa Nne: Sh. Milioni 21
  Mfungaji Bora: Sh. Milioni 5.2
  Timu yenye Nidhamu; Sh. Milioni 16
  Kipa Bora: Sh. Milioni 5.2
  Refa Bora; Sh. milioni 5.2
  Mwalim amesema mabingwa Azam FC watazawadiwa Sh. milioni 75 ikiwa ni ongezeko la Sh. milioni 5 ikilinganishwa na ilivyokuwa msimu uliopita. Kipa bora, mwamuzi bora watapata Sh. milioni 5.2 kila mmoja ikikwa ni ongezeko la Sh. 200,000.
  Timu yenye nidhamu italamba Sh. milioni 16, ikiongezeka kutoka Sh. 15 ya msimu uliopita zilizochukuliwa na Yanga.
  Silas Mwakibinga, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu (TPLB), aliyekuwa amefuatana na Mwalim kwenye mkutano huo na waandishi wa habari, alisema tarehe ya kutolewa kwa tuzo hizo itatangazwa baada ya wiki moja.
  "Tumejipanga kuhakikisha utoaji wa tuzo mwaka huu unakuwa mzuri zaidi, vipengele vya kushindaniwa (ambavyo havina washindi wa moja kwa moja) vitakuwa na watu watatu ambao wote watakuwapo kwenye utoaji wa tuzo," amesema Mwakibinga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: VODACOM KUWAJAZA MABINGWA AZAM FC MILIONI 100 KASORO KIDOGO, TAMBWE KUPEWA MILIONI 5 NA UPUUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top