• HABARI MPYA

  Ijumaa, Aprili 25, 2014

  SKWADI JIPYA LA KAZI MAN UNITED

  Watauweza mfupa uliomshinda fisi? Benchi jipya la Ufundi la Manchester United kutoka kushoto Phil Neville, Nicky Butt, Paul Scholes na bosi wao, Ryan Giggs katika picha ya pamoja kabla ya mazoezi leo kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Norwich City kesho. Giggs ameteuliwa kuwa kaimu kocha mkuu wa United, baada ya kutimuliwa kwa David Moyes wiki hii kufuatia matokeo mabaya. Je, timu hii mpya ya benchi la Ufundi itarejesha furaha kwa Mashetani Wekundu?
  Wasifu wao; 
  Phil Neville: Alijiunga na Man United mwaka 1992 na hadi anastaafu aliichezea mechi 386, akishinda mataji 10, la Kombe Ligi moja, Ligi Kuu sita na Kombe la FA matatu.
  Nicky Butt: Alijiunga na Man United mwaka 1991 na hadi anastaafu aliichezea mechi 387 akishinda mataji 10, Kombe la Ligi moja, Ligi Kuu sita na Kombe la FA matatu.  
  Paul Scholes: Alijiunga na Man United mwaka 1991 na hadi anastaafu ameichezea mechi 718 akishinda mataji 18, mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, 11 ya Ligi Kuu, matatu ya FA na mawili ya Kombe la Ligi.
  Ryan Giggs: Alijiunga na Man United mwaka 1987 na hadi sasa ameichezea mechi 962, ameshinda mataji 23, mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, 13 ya Ligi Kuu, manne ya FA na manne ya Kombe la Ligi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SKWADI JIPYA LA KAZI MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top