• HABARI MPYA

  Ijumaa, Aprili 25, 2014

  KOCHA WA BARCA TITO VILANOVA AFARIKI DUNIA

  KOCHA wa zamani wa Barcelona, Tito Vilanova amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 45 baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani kwa muda mrefu.
  Alipelekwa chumba cha dharula jana kwa upasuaji baada ya hali yake kugeuka na kuwa mbaya wiki iliyopita. 
  Vilanova amekuwa akisumbuliwa na saratani tangu Novemba mwaka 2011 na Radio Nacional imesema alikuwa katika wakati mgumu siku mbili hizi.
  Gwiji: Tito Vilanova amefariki dunia akiwa na umri wa miakia 45 baada ya kusumbuliwa na saratani kwa muda mrefu 

  Klabu hiyo ya Katalunya imetweet: "FC Barcelona ipo katika huzuni. Tito Vilanova amefariki akiwa na umri wa miaka 45. Apumzike kwa amani,".
  Winner: Vilanova (left) and Eric Abidal (right) lift the La Liga trophy together in 2013
  Washindi: Vilanova (kushoto) na Eric Abidal (kulia) wakiinua taji la La Liga mwaka 2013

  Kocha huyo alilazimika kujiuzulu mwaka 2013 baada ya kuanza kuzidiwa na maradhi hayo. 
  Timu yake ilishinda taji la La Liga, lakini Jordi Roura aliifundisha Barcelona kwa miezi miwili wakati Vilanova aliposafiri kwenda New York kwa matibabu ya saratani, kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Tata Martino msimu huu. 
  Vilanova aliteuliwa kuwa kocha wa Barcelona mwishoni mwa msimu wa 2011-12 na akawawezesha Blaugrana kusawazisha rekodi ya Real Madrid kumaliza msimu na pointi 100. Alianza kuwa Msaidizi wa Pep Guardiola mwaka 2008.

  WASIFU WA TITO VILANOVA...

  1968: Kuzaliwa Septemba 17 mjini Bellcaire d'Emporda, kijiji kilichopo Katalunya.
  1988: Alijiunga na timu ya vijana ya Barcelona pamoja na kiungo mwenzake Pep Guardiola, lakini hakupanda kikosi cha kwanza akichezea kwa miaka miwili Barcelona B.
  1990: Alijiunga na timu ya daraja la chini Figueres.
  1992: Alihamia timu ya La Liga, Celta Vigo, lakini akashindwa kupata nafasi kikosi cha kwanza.
  1995: Aliondoka Celta.
  2002: Alistaafu soka baada ya kucheza madaraja ya chini katimu za Badajoz, Real Mallorca, Lleida, Elche na hatimaye Gramenet.
  2007: Baada ya kufanya kazi kama Mkurugenzi wa Ufundi wa Tarrassa, Vilanova akateuliwa kuwa Msaidizi wa Guardiola Barcelona B, ambao kwa pamoja waliiwezesha timu hiyo kupanda daraja la pili.
  Success: Vilanova helped Barcelona lift their 22nd La Liga title in 2013
  2008: Juni - Guardiola alipewa Ukocha Mkuu wa Barcelona na Vilanova akawa Msaidizi wake. Wawili hao walishinda taji la Kombe la Mfalme, La Liga na Ligi ya Mabingwa katika msimu wao wa kwanza kazini. Mataji mawili zaidi ya ligi, lingine la Ligi ya Mabingwa na mawili ya Klabu Bingwa ya Dunia yalifuatia.
  2011: Novemba 22 - alikwenda kufanyiwa upasuaji wa kwanza wa matatizo yake ya kiafya akiwa Barcelona na akatumia wiki tatu kabla ya kupona na kurejea kazini.
  2012: Aprili 27 - Aliteuliwa kuwa kocha mpya wa Barcelona, baada ya Guardiola kutangaza hataongeza mkataba.
  Juni 15 - Vilanova alisani Mkataba wa miaka miwili .
  Desemba 19 - Barcelona ilitangaza Vilanova atakwenda kufanyiwa upasuaji kwa mara ya pili na atakosekana kwa wiki sita.
  2013: Machi 26 - Baada ya wiki 10 za matibabu New York, Marekani Vilanova alirejea Barcelona.
  Aprili 6 - Alirejea Uwanja wa Nou Camp akiiongoza timu hiyo kushinda 5-0 nyumbani dhidi ya Real Mallorca.
  Aprili 26 - Alizungumza na vyombo vya habari kwa mara ya kwanza baada ya matibabu yake, akisema: "Najisikia mwenye furaha na nguvu na ninataka kuendelea msimu ujao."
  Mei 11 - Barcelona ilitwaa taji la 22 la La Liga baada ya wapinzani wao, Real Madrid kukamatwa kwa sare na Espanyol.
  Julai 19 - Barcelona ilitangaza kung'atuka kwa Vilanova ili kuendelea na matibabu.
  2014: Aprili 25 - Barcelona ilitangaza kifo cha Vilanova akiwa na umri wa miaka 45.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KOCHA WA BARCA TITO VILANOVA AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top