• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 24, 2014

  LOGARUSIC AONGEZEWA MKATABA SIMBA SC, YAW BERKO ATUPIWA VIRAGO

  Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
  KOCHA wa Simba SC, Zdravko Logarusic aondoka leo kwenda mapumzikoni nyumbani kwao Croatia, baada ya kukubaliana na uongozi wa klabu hiyo kuendelea kuifundisha timu hiyo.
  BIN ZUBEIRY inafahamu Logarusic alikuwa na kikao leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya timu hiyo, Zacharia Hans Poppe na amepewa stahiki zake zote kuelekea likizo hadi Juni.
  “Logarusic ataendelea na kazi Simba SC, ni mwalimu ambaye wadau wote wa timu yetu wamemkubali na wameona bora wampe muda zaidi kuona na msimu ujao atavuna nini,”kimesema chanzo kutoka Simba SC.

  Bado yupo yupo: Kocha Zdravko Logarusic anaondoka leo kwenda likizo kwao Croatia, lakini atarejea kuendelea na kazi Simba SC 

  REKODI YA LOGARUSIC SIMBA SC;

  Simba SC 3-1 KMKM (Kirafiki)
  Simba SC 3-1 Yanga SC (Mtani Jembe) 
  Simba SC 1-0 KMKM (Kombe la Mapinduzi)
  Simba SC 2-0 Chuoni (Robo Fainali Mapinduzi)
  Simba SC 2-0 URA (Nusu Fainali Mapinduzi)
  Simba SC 0-1 KCC (Fainali Kombe la Mapinduzi)
  Simba SC 0-1 Mtibwa Sugar (Kirafiki)
  Simba SC 1-0 Rhino Rangers (Ligi Kuu Bara)
  Simba SC 4-0 JKT Oljoro (Ligi Kuu Bara)
  Simba SC 1-1 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu Bara)
  Simba SC 0-1 Mgambo JKT (Ligi Kuu Bara)
  Simba SC 1-1 Mbeya City (Ligi Kuu Bara)
  Simba SC 2-3 JKT Ruvu (Ligi Kuu Bara)
  Simba 3-2 Ruvu Shooting (Ligi Kuu Bara)
  Simba SC 0-0 Prisons (Ligi Kuu Bara)
  Simba SC 0-1 Coastal Union (Ligi Kuu)
  Simba SC 1-2 Azam FC (Ligi Kuu)
  Simba SC 1-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu)
  Simba SC 0-1 Ashanti United (Ligi Kuu)
  Simba SC 1-1 Yanga SC (Ligi Kuu)
  Kwa upande mwingine, kipa Mghana Yanga Berko yeye hataongezewa Mkataba baada ya kumaliza Mkataba wake wa wa miezi sita.
  Simba SC inaachana na Berko ili kusajili kipa mzalendo na kutoa nafasi za wachezaji wa ndani wa kigeni.
  Mabeki Mkenya Donald Mosoti na Mganda Joseph Owino wote wataongezewa mikataba na mshambuliaji Mrundi Amisi Tambwe, wakati mwenzake Kaze Gilbert ameonyeshwa mlango wa kutokea.
  Nje; Yaw Berko amefungwa mabao sita katika mechi tano na kwa sababu hiyo haongezwi mkataba

  REKODI YA YAW BERKO SIMBA SC

  Simba SC 3-1 KMKM (Kirafiki, alifungwa moja Dar)
  Simba SC 1-0 KMKM  (Kombe la Mapinduzi, hakufungwa) 
  Simba SC 0-1 Mtibwa Sugar (Kirafiki, alifungwa moja)
  Simba SC 1-1 Mbeya City (Ligi Kuu Bara, alifungwa moja)
  Simba SC 2-3 JKT Ruvu (Ligi Kuu Bara, alifungwa tatu)
  Orodha ya wachezaji wa kuongeza kikosini kwa ajili ya msimu ujao tayari Logarusic amekwishaiwasilisha kwa Hans Poppe ambaye anaanza kuifanyia kazi kuanzia kesho. 
  Logarusic aliyejiunga na Simba SC Desemba mwaka jana, amekwishaiongoza timu hiyo katika mechi 20 za mashindano yote, akiiwezesha kushinda mechi nane, sare tane na kufungwa saba, wakati Berko ameidakia Simba SC mechi tano na kufungwa jumla ya mabao sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LOGARUSIC AONGEZEWA MKATABA SIMBA SC, YAW BERKO ATUPIWA VIRAGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top