• HABARI MPYA

  Jumatano, Aprili 23, 2014

  REAL YAPATA USHINDI MWEMBAMBA WA MBINDE DHIDI YA BAYERN

  BAO pekee la Karim Benzema limeipa Real Madrid ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Bayern Munich usiku huu katika Nusu Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Hispania.
  Benzema alifunga bao hilo dakika ya 19 baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Cristiano Ronaldo, ambaye hakuwa na bahati leo kwa kukosa mabao mengi ya wazi.
  Mshindi wa mechi; Karim Benzema akishangilia baada ya kufunga bao pekee dhidi ya Bayern

  Real sasa itakuwa na kibarua kizito wiki ijayo katika mchezo wa marudiano ikitakiwa kuulinda ushindi huo mwembamba mbele ya mabingwa hao watetezi wa Ulaya.
  Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Howard Webb wa England, Ronaldo aliyecheza akiwa majeruhi alimpisha Gareth Bale dakika ya 73 ambaye aliripotiwa kusumbuliwa na mafua kabla ya mchezo huo.
  Vikosi vilikuwa, Real Madrid: Casillas, Carvajal, Sergio Ramos, Pepe/Varane dk73, Fabio Coentrao, Modric, Alonso, Di Maria, Isco/Illarramendi dk82, Benzema na Ronaldo/Bale dk73.
  Bayern Munich: Neuer, Rafinha/Javi Martinez dk66, Boateng, Dante, Alaba, Lahm, Schweinsteiger/Muller dk74, Robben, Kroos, Ribery/Gotze dk72 na Mandzukic.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: REAL YAPATA USHINDI MWEMBAMBA WA MBINDE DHIDI YA BAYERN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top