• HABARI MPYA

  Jumamosi, Aprili 19, 2014

  IVO, CANNAVARO WATEMWA STARS, MAKIPA WOTE WA AZAM WACHUKULIWA

  Na Waandishi Wetu, Dar es Salaam
  KOCHA Msaidizi wa Taifa Stars, Salum Mayanga amewaacha kipa Ivo Mapunda wa Simba SC na beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wa Yanga SC katika kikosi chake cha wachezaji wengine 23 watakaoingia kambini kesho (Aprili 20 mwaka huu) kuungana na 16 waliotajwa awali kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi itakayochezwa Aprili 26 mwaka huu.
  Mayanga amewaita makipa wote wa Azam FC, Aishi Manula na Mwadini Ally pamoja na Deogratias Munishi wa Yanga, wakati mabeki aliowachukua ni Abdi Banda (Coastal Union), Aidan Michael (Ruvu Shooting), Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Hassan Mwasapili (Mbeya City), Kelvin Yondani (Yanga SC)na Said Moradi (Azam).
  Ametemwa; Kipa wa Simba SC, Ivo Mapunda ameachwa Taifa Stars

  Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Frank Domayo (Yanga), Himid Mao (Azam) na Jonas Mkude (Simba).
  Washambuliaji ni Athanas Mdamu (Alliance), Haruna Chanongo (Simba), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Khamis Mcha (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngassa (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Markhiya, Qatar), Ramadhan Singano (Simba), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
  Wachezaji walioitwa kutoka katika kikosi cha maboresho ni kipa Benedicto Tinoko Mlekwa (Mara), mabeki wa kati; Emma Namwondo Simwanda (Temeke) na Joram Nason Mgeveje (Iringa). Walinzi wa pembeni ni Omari Ally Kindamba (Temeke), Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba) na Shiraz Abdallah Sozigwa (Ilala).
  Viungo ni Yusuf Suleiman Mlipili (Temeke), Said Juma Ally (Mjini Magharibi), Abubakar Ally Mohamed (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magona (Shinyanga), Omari Athumani Nyenje (Mtwara) na Chunga Said Zito (Manyara).
  Simon Msuva kulia ameitwa, Cannavaro kushoto ametemwa

  Washambuliaji ni Mohammed Seif Saidi (Kusini Pemba), Ayoub Kasim Lipati (Ilala), Abdurahman Othman Ally (Mjini Magharibi), Paul Michael Bundara (Ilala). Wachezaji wa U 20 ni Mbwana Mshindo Musa (Tanga) na Bayaga Athanas Fabian (Mbeya).
  Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaingia kambini kwenye hoteli ya Kunduchi Beach.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: IVO, CANNAVARO WATEMWA STARS, MAKIPA WOTE WA AZAM WACHUKULIWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top