• HABARI MPYA

  Jumapili, Aprili 27, 2014

  TAIFA STARS ILIVYOCHAPWA 'SERIKALI TATU' JANA TAIFA NA DIDA LANGONI

  Wa Jangwani; Kiungo wa Tanzania, Taifa Stars, Frank Domayo akimtoka mshambuliaji wa Burundi, Didier Kavumbangu anayecheza naye klabu moja, Yanga SC katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa jana Uwanja wa Taifa Dar es Salaam uliokwenda sambamba na sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Burundi au Int'hamba Murugamba ilishinda mabao 3-0.
  Mshambuliaji wa Burundi, Amisi Cedric akimtoka winga wa Tanzania, Simon Msuva
  Ramadhani Singano 'Messi' wa Tanzania akichuana na Steve Nzigamasabo wa Burundi kulia
  Nahodha wa Burundi, Didier Kavumbangu kushoto akimtoka Nahodha wa Tanzania, Aggrey Morris
  Mshambuliaji wa Burundi,Amisi Tambwe kushoto akitoa pasi pembeni ya beki wa Tanzania, Said Mourad
  Chipukizi wa Tanzania, Ayoub Lipati akitia krosi pembeni ya beki wa Burundi, Rashid Leon
  Mashabiki wa Tanzania wakiwa wenye huzuni baada ya bao la tatu
  Kocha mpya wa Tanzania, Mart Nooij raia wa Uholanzi aliyewasili jana, alikuwepo Taifa kushuhudia timu yake mpya ikifungwa 3-0
  Kikosi cha Burundi kilichoiadhibu Stars jana
  Kikosi cha Tanzania kilichochapwa 3-0 jana
  Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kulia akimfariji beki wa Azam FC, Samih Haji Nuhu ambaye ametoka kufanyiwa upasuaji wa goti hivi karibuni nchini Afrika Kusini. Kushoto kwa beki huyo wa timu ya taifa pia,ni Rais wa Shirikisho la Soka Burundi (FFB), Reverien Ndikuriyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TAIFA STARS ILIVYOCHAPWA 'SERIKALI TATU' JANA TAIFA NA DIDA LANGONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top