• HABARI MPYA

    Friday, April 18, 2014

    WAZOEFU TAIFA STARS KUTAJWA KESHO

    Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
    WACHEZAJI wazoefu wa Taifa Stars watakaoungana na wale 16 waliopatikana katika mpango wa maboresho wa timu hiyo watatangazwa kesho (Aprili 19 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
    Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itapiga kambi kwenye hoteli ya Kunduchi Beach kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi itakayochezwa Aprili 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Wachezaji waliopatikana katika mpango wa maboresho ya Stars wanatarajiwa kuwasili leo (Aprili 18 mwaka huu), na kwenda moja kwa moja kambini kuwasubiri wenzao watakaotajwa kesho (Aprili 19 mwaka huu).
    Ataitwa? Simon Msuva amekuwa katika kiwango kizuri mwaka huu, je atarejeshwa Taifa Stars 

    Wachezaji hao ni kipa Benedicto Tinoko Simwanda (Mara), Emma Namwondo Simwanda (Temeke), Joram Nason Mgeveje (Iringa), Omari Ally Kindamba (Temeke), Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba), Shiraz Abdallah Sozigwa (Ilala), Yusuf Suleiman Mlipili (Temeke) na Said Juma Ally (Mjini Magharibi).
    Wengine ni Abubakar Ally Mohamed (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magona (Shinyanga), Omari Athumani Nyenje (Mtwara), Chunga Said Zito (Manyara), Mohammed Seif Saidi (Kusini Pemba), Ayoub Kasim Lipati (Ilala), Abdurahman Othman Ally (Mjini Magharibi) na Paul Michael Bundara (Ilala).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAZOEFU TAIFA STARS KUTAJWA KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top