• HABARI MPYA

  Jumamosi, Aprili 26, 2014

  GIGGS AANZA NA 4-0 MAN UNITED

  RYAN Giggs ameanza vizuri kazi ya ukocha Manchester United akirithi mikoba ya David Moyes baada ya jioni hii kuwawezesha Mashetani hao Wekundu kuwalaza Norwich City mabao 4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
  Wayne Rooney na Juan Mata kila mmoja alifunga mabao mawili na sasa United inatimiza pointi 60 baada ya kucheza mechi 35, ingawa inabaki nafasi ya saba, nyuma ya Tottenham Hotspur yenye pointi 66 ambayo hata hivyo imecheza mechi moja zaidi.  

  Rooney alifunga bao la kwanza kwa penalti dakika ya 41 na la pili akimalizia pasi ya Shinji Kagawa dakika ya 48, wakati Mata alifunga dakika ya 63 kwa pasi ya Phil Jones na dakika ya 73 kwa pasi ya 
  Antonio Valencia.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu ya England zilizochezwa mapema leo, Southampton imeichapa 2-0 Everton, Fulham imetoka sare ya 2-2 na Hull City, Stoke City imefungwa 1-0 nyumbani na Tottenham Hotspur, Swansea City imeichapa 4-1 Aston Villa na West Bromwich imeilaza 1-0 West Ham United.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: GIGGS AANZA NA 4-0 MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top