• HABARI MPYA

  Ijumaa, Aprili 25, 2014

  MAJARIBIO AZAM AKADEMI YASOGEZWA MBELE

  Na Prince Akbar, Dar es Salaam
  MAJARIBIO ya kusaka vipaji vya kujiunga na akademi ya Azam FC ambayo hufanyika kila tarehe ya mwanzo ya mwezi, hayatakuwepo kwa miezi ya Mei na Juni, mwaka huu.
  Kocha Mkuu wa Azam Academy, Vivek Nagul raia wa India amekaririwa na tovuti ya klabu hiyo akisema majaribio yafuatayo yatafanyika Julai 1 mwaka huu kuanzia Saa 12.30 asubuhi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Kocha Mkuu wa Azam Akademi, Vivek Nagul kushoto akiwa na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza cha Azam FC, Mcameroon Joseph Marius Omog kulia
  Vivek ameomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza na amewataka vijana wenye ndoto za kujiunga na akademi hiyo kujitokeza Julai 1 kujaribu bahati yao. “Wazazi pia, ambao wana ndoto za kuwaleta vijana wao hapa, tunapenda kuwaambia nafasi nyingine kwao ni Julai 1, wanakaribishwa,”alisema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAJARIBIO AZAM AKADEMI YASOGEZWA MBELE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top