• HABARI MPYA

  Jumamosi, Aprili 19, 2014

  RONALDO FITI KUICHEZEA REAL MADRID DHIDI YA BAYERN MUNCH JUMATANOA

  MWANASOKA bora waq dunia, Cristiano Ronaldo jana alianza mazoezi na wenzake Real Madrid akipambana kuwa fiti kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa nyumbani dhidi ya Bayern Munich Jumatano.
  Matatizo ya goti na misuli yalimuweka nje mshindi huyo wa Ballon d'Or winner na kukosa mechi nne za Real, ikiwemo fainali ya Copa del Rey Jumatano wiki hii timu yake ikiifunga Barcelona 2-1 katika mchezo ambao Gareth Bale alifunga bao la ushindi.
  Kurejea kwa Ronaldo ni faraja kwa mashabiki wa Real ambao hawajamuona mchezaji huyo tangu alipoumia katika mechi ya kwanza ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Borussia Dortmund.


  Matumaini: Ronaldo anaweza kucheza dhidi ya mabingwa Ulaya, Bayern Munich Jumatano
  Battle: The Ballon d'Or winner is racing the clock to overcome knee and thigh problems
  Mshindi huyo wa Ballon d'Or anapambana kuwa fiti ili acheze


  Ronaldo anayeongoza kwa mabao La Liga na Ligi ya Mabingwa msimu huu,anamuongezea matumaini kocha wa Real, Carlo Ancelotti kuelekea mechi na Bayern huku Real ikipigania taji la 10 la michuano hiyo na la kwanza tangu walipotwa mara ya mwisho, mwaka 2002.
  Ronaldo na beki wa kushoto Mbrazil, Marcelo, ambaye pia alikuwa majeruhi wote walianza mazoezi jana. Real itacheza mechi ya marudiano na Bayern mjini Munich Aprili 29 na mshindi wa jumla atakutana na akti ya Atletico Madrid au Chelsea kwenye fainali Mei 24.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RONALDO FITI KUICHEZEA REAL MADRID DHIDI YA BAYERN MUNCH JUMATANOA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top