• HABARI MPYA

  Ijumaa, Aprili 25, 2014

  TEVEZ AIFUNGIA BAO MUHIMU JUVENTUS EUROPA LEAGUE, SEVILLA YAICHAPA 2-0 VALENCIA

  BAO la dakika za mwishoni la Lima limeipa ushindi mwembamba Benfica katika Nusu Fainali ya kwanza ya Europa League dhidi ya Juventus usiku wa kuamkia leo. 
  Benfica sasa itakuwa na mtihani wa kuulinda ushindi huo katika mchezo wa marudiano dhidi ya vigogo hao wa Serie A wiki ijayo mjini Turin. Juve inawania taji la kwanza la Ulaya baada ya miaka 17. 
  Lima alipokea pasi ndani ya boksi na kuwafungia wenyeji bao la ushindi dakika ya 84, baada ya Carlos Tevez kutoka kuisawazishia Juve dakika ya 72 katika mchezo ambao beki wa kati Ezequiel Garay alitangulia kuifungia Benfica bao la kuongoza dakika ya pili. 
  Katika mchezo mwingine wa Nusu Fainali ya michuano hiyo, Sevilla imeifunga Valencia 2-0, mabao ya Mbia dakika ya 33 na Bacca dakika ya 66.
  Bao muhimu; Carlos Tevez akishangilia baada ya kuifungia bao la ugenini Juventus ikilala 2-1 Benfica
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TEVEZ AIFUNGIA BAO MUHIMU JUVENTUS EUROPA LEAGUE, SEVILLA YAICHAPA 2-0 VALENCIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top