• HABARI MPYA

  Jumatano, Aprili 30, 2014

  POLISI PWANI YACHAPA TANESCO 3-0

  Na Mwandishi Wetu, Kibaha 
  Timu ya polisi mkoa wa pwani jana imeibuka kidedea kwenye mchezo maalum wa kuadhimisha sherehe za wafanyakazi za Mei Mosi kwa kuifunga tanesco ya mkoa huo kwa mabao 3-0
  Mchezo huo uliovuta mashabiki wengi ulifanyika katika uwanja wa shirika la elimu kibaha mkoani pwani 
  Polisi iliyong'ara zaidi kupitia kiungo w a zamani Robert Munishi 'Baggio' walionekana kuwamudu vema wapinzani wao kwa kucheza kandanda safi na la kuvutia.
  Robert Munishi kushoto

  Mshambuliaji Shaaban Mkwinda sambamba na Raymond aliyefunga mabao miwili waliweza kuzima kelele za Tanesco kwenye dakika 90 za mchezo huo.
  Kwa ushindi huo Polisi imeingia fainali ambapo itapambana na shirika la elimu katika mchezo wa kufunga michuano hiyo. Shirika la elimu limeingia fainali baada ya kuwafunga chama cha walimu mabao 5-0.
  Mchezo huo wa fainali utafanyika kwenye Uwanja wa shirika la elimu mkoani, Kibaha.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: POLISI PWANI YACHAPA TANESCO 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top