• HABARI MPYA

  Jumanne, Aprili 29, 2014

  MALAWI KUWASILI MEI 1 KUIVAA STARS

  Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
  TIMU ya Taifa ya Malawi (Flames) inatarajiwa kuwasili nchini Mei 1 mwaka huu kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Mei 4 mwaka huu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
  Flames yenye msafara wa 31 utakaoongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Mpira wa Miguu cha Malawi (FAM) utaingia Mbeya kwa usafiri wa barabara. Wachezaji katika msafara huo ni 20.
  Makinda wa maboresho ya Stars watachanganyika na wakongwe kumenyana na Malawi

  Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ikiwa chini ya Kocha mpya, Mart Nooij tayari ipo jijini Mbeya kujiwinda kwa mechi hiyo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya mashindano dhidi ya Zimbabwe itakayochezwa jijini Dar es Salaam kati ya Mei 16 na 18 mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MALAWI KUWASILI MEI 1 KUIVAA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top