• HABARI MPYA

  Jumatatu, Aprili 21, 2014

  MOYES NI WA KUFUKUZWA WAKATI WOWOTE MAN UNITED

  WAMEMCHOKA! Wamiliki wa klabu ya Manchester United, Familia ya Glazer wamechoshwa na mwenendo mbovu na sasa kibarua cha kocha wao, David Moyes kiko mashakani na wamepanga kumtimua wakati wowote kuanzia usiku huu.
  Bodi ya Klabu hiyo ikiongazwa na wamiliki Falimia ya Glazer ipo kwenye kikao kizito kujadili mustakabali wa Moyes Old Trafford.
  Familia ya Glazer imechoshwa na kufungwa kila wiki kwenye Ligi Kuu England, huku timu hiyo ikikamata nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi hiyo.
  Mwisho wake umewadia: David Moyes anaweza kufukuzwa Manchester United kabla ya msimu kumalizikaUnder pressure: United crashed to a 2-0 defeat at Moyes's former club Everton on Sunday, their 11th defeat of the Premier League season
  Kuti kavu: United ilifungwa 2-0 dhidi ya timu ya zamani ya Moyes, Everton jana katika Ligi Kuu ya England

  DAVID MOYES MAN UNITED

  Amecheza mechi 51
  Ameshinda mechi 27
  Ametoa sare mechi 9
  Amefungwa mechi 15
  Asilimia ya ushindi ni 52.94
  Kichapo cha juzi cha mabao 2-0 kutoka kwa Everton ndicho kilihitimisha maisha ya Moyes United kwa sababu kilimaanisha timu hiyo ilikuwa imepoteza mechi yake ya 11 msimu huu na wako nyuma kwa pointi 13 kutoka katika nafasi ya nne,
  Familia ya Glazer na Mtendaji Mkuu wa United, Ed Woodward walikuwa wamepania kumvumilia Moyes, lakini wameona kiwango cha timu yao kinazidi kuporomoka kila wiki na wachezaji wanaonekana kuacha kujitoa kwa ajili ya kocha wao.
  Imefahamika kwamba mpango uliokuwepo ni kumtimua Moyes mwisho wa msimu, lakini hali ilivyo kulikuwa na kila dalili kwamba alitarajiwa kutimuliwa usiku wa kuamkia leo au siku cheche zijazo. Kama Moyes akitimulia gwiji wa klabu hiyo Ryan Giggs anatarajiwa kuombwa kuongoza kwa muda.
  Huku makocha Jurgen Klopp wa Borussia Dortmund, Louis van Gaal wa Uholanzi na Carlo Ancelotti wa Real Madrid wakitajwa kuja kuchukua ukocha wa kudumu.
  Licha ya usajili wa fedha nyingi kwa Marouane Fellaini wakati wa kiangazi na Juan Mata, Januari, United imeshindwa kupambana na wapinzani wao kwenye mbio za ubingwa.
  Moyes ambaye alirithi mikoba ya Sir Alex Ferguson wakati wa kiangazi, pia amechemka kwenye michuano mingine msimu huu, United ilitolewa na Swansea City katika hatua ya tatu ya Kombe la FA, wakati Sunderland waliwatoa kwenye nusu fainali ya Kombe la Ligi na Bayern Munich kwenye Ligi ya Mabingwa.
  Katika michuano yote Moyes kashinda mechi 27 kati ya 51 akitoka sare mara nane na kufungwa mara 15.
  Watu wanaamini kuwa Ferguson anaweza kuchukua mikoba ya kuinoa timu hiyo kwa muda hadi pale kocha mpya atakapopatikana, huku Giggs naye akipewa nafasi kubwa ya kumrithi Moyes.

  MECHI ZILIZOBAKI

  Aprili 26 Norwich City (nyumbani)
  Mei 3 Sunderland (nyumbzani)
  Mei 6 Hull City (nyumbani)
  Mei 11 Southampton (ugenini)
  Katika hatua nyingine uongozi wa Manchester United chini ya Familia ya Glazer na Ed Woodward, ulikuwa umeshapata majina matatu ya makocha wakubwa  ambao wamekuwa na mafanikio makubwa msimu huu, ambapo jina la kwanza na ambalo linapigiwa chapuo kubwa ni la Jurgen Klopp ambapo uongozi wa Man umekubali kulipa fedha kwa ajili ya kuvunja mkataba wake mrefu na Borussia Dortmund .
  Kocha mwingine Laurant Blanc ambaye amewahi kucheza United na kwa ni kocha Paris Saint-Germain, -(PSG) mabingwa wapya wa Ufaransa. Hata hivyo uongozi wa United umekiri kuwepo kwa ugumu wa kumpata Blanc kutokana na mkataba wake, ingawa wanaamini anaweza kuvutiwa na uzalendo wake kwa timu hiyo ya Old Trafford.
  Diego Simeone anayetamba hivi sasa na Atletico Madrid, naye yumo katika orodha hiyo ya kuchukua nafasi ya Moyes, na uongozi huo umesema hawatakuwa na pingamizi lolote kuvunja benki kwa ajili ya kumpata mtu sahihi kwa mafanikio ya United.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MOYES NI WA KUFUKUZWA WAKATI WOWOTE MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top