• HABARI MPYA

  Jumamosi, Aprili 19, 2014

  DIEGO COSTA ACHEZA DAKIKA ZOTE 90 NA KUFUNGA ATLETICO IKIUA 2-0 NA KUUSOGELEA UBINGWA LA LIGA

  MABAO ya Joao Miranda kwa kichwa na Diego Costa kwa penalti yameiwezesha Atletico Madrid kuusogelea ubingwa wa Hispania baada ya usiku wa jana kuilaza 2-0 Elche katika La Liga
  Ushindi huo unakuja siku chache kabla ya vinara hao wa La Liga kucheza mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Chelsea.
  The Blues itamenyana na Atletico Uwanja wa Vicente Calderon katika Nusu Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa usiku wa Jumanne.
  Kikosi cha Diego Simeone sasa kipo kileleni kwa pointi zake 85 baada ya kucheza 34, kikifuatiwa na Real Madrid pointi 79 mechi 33 na Barcelona pointi 78 mechi 33 pia.
  Diego Costa alicheza dakika zote 90 licha ya kuchanika nyama ya ugoko baada ya kujigonga kwenye nguzo ya lango mwishoni mwa wiki iliyopita.
  Mambo safi: Atletico Madrid imepanda kileleni kwa pointi sita zaidi baada ya jana kuifunga Elche 2-0
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DIEGO COSTA ACHEZA DAKIKA ZOTE 90 NA KUFUNGA ATLETICO IKIUA 2-0 NA KUUSOGELEA UBINGWA LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top