• HABARI MPYA

  Jumanne, Aprili 29, 2014

  BARCELONA ILISIMAMA USIKU WA JANA KWA MAZISHI YA MPENDWA WAO TITO VILANOVA

  SKWADI zima la Barcelona usiku wa jana limeuaga mwili wa aliyekuwa kocha wao, Tito Vilanova kabla ya mazishi yake.
  Wachezaji wa kikosi cha kwanza walihudhuria ibada ya kuuaga mwili wa marehemu katika kanisa la Cathedral mjini Barcelona na kutoa heshima zao za mwisho kwa Vilanova, aliyefariki dunia Ijumaa akiwa na umri wa miaka 45 baada ya kusumbuliwa na maradhi saratani.
  Mkewe na watoto wao wawili wa kike pia walihudhuria pamoja na mtoto wao kiume, Adria, anayechezea akademi ya Barca, na binti yake Carlota, alilia sana.
  Heshima za mwisho: Kutoka kushoto, Victor Valdes, Carles Puyol, Xavi na Andres Iniesta wakiwa katika ibada ya kuuaga mwili wa Tito Vilanova
  Sad day: Barcelona's Brazilian defender Dani Alves (left) and Neymar stand during the religious ceremony
  Dani Alves (kushoto) na Neymar kulia
  For you: Star striker Lionel Messi scored for Barca on Sunday before dedicating his goal to Vilanova
  Lionel Messi alikuwepo pia kumuaga Vilanova
  Legend: Tito Vilanova has passed away at the age of 45 after losing his battle with throat cancer
  Pumzika kwa amani: Tito Vilanova amefariki akiwa kijana wa miaka 45

  Ibada hiyo iliongozwa na Mchungaji wa Barcelona, Lluis Martinez Sistach.
  Marais wa zamani wakiwemo Joan Laporta na Sandro Rosell walikuwepo kanisani, pamoja na Wajumbe wa bodi walioongozwa na Rais wa sasa, Josep Maria Bartomeu.
  "Leo tunamuaga mpendwa wetu,"alisema Bartomeu. "Nakuahidi, daima atadumu katika mioyo yetu na hatutamsahau milele,"aliongeza.
   Goodbye: Barca coach Gerardo Martino was also in attendance at the Barcelona Cathedral
   President of FC Barcelona Josep Maria Bartomeu
   Kwaheri: Gerardo Martino (kushoto) na Rais wa Barca, Josep Maria Bartomeu pia walikuwepo
   Emotional: Mourners gather at the stunning cathedral in the heart of Barcelona
   Waombolezaji mbalimbali wakiwa kanisani jana
   Support: Barca keeper Victor Valdes arrives on crutches after undergoing surgery to his knee injury
   Kipa wa Barca, Victor Valdes akiwasili na 'magongo' yake baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti aliloumia
   • Blogger Comments
   • Facebook Comments

   0 maoni:

   Item Reviewed: BARCELONA ILISIMAMA USIKU WA JANA KWA MAZISHI YA MPENDWA WAO TITO VILANOVA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
   Scroll to Top