• HABARI MPYA

  Jumapili, Aprili 27, 2014

  NOOIJ AWAONGEZA BOCCO, KAPOMBE NA JAVU STARS, AMETAMA YONDAN

  Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
  KOCHA mpya wa Taifa Stars, Mart Nooij ameongeza wachezaji tisa katika kikosi hicho kinachojiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Malawi (The Flames) itakayochezwa Mei 4 mwaka huu katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
  Wachezaji walioongezwa ni Edward Charles Manyama (JKT Ruvu), Elias Maguli (Ruvu Shooting), Hassan Dilunga (Yanga), Hussein Javu (Yanga), John Bocco (Azam), Kelvin Friday (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Nadir Haroub (Yanga) na Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa).
  Wameongezwa; John Bocco kushoto na Shomary Kapombe kulia wameongezwa Stars

  Naye beki Kelvin Yondani wa Yanga ambaye aliitwa awali ameondolewa katika kikosi hicho kwa vile ameshindwa kuripoti kambini.
  Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Pemium Lager inaingia kambini kesho (Aprili 28 mwaka huu) jijini Mbeya kujiandaa kwa mechi dhidi ya Malawi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NOOIJ AWAONGEZA BOCCO, KAPOMBE NA JAVU STARS, AMETAMA YONDAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top