• HABARI MPYA

  Jumatano, Aprili 23, 2014

  DIEGO COSTA AWAPA ISHARA NZURI CHELSEA...NI DALILI ZA KUHAMIA DARAJANI

  MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid, Diego Costa anaweza kuwa katika jaribio la kuing'oa Chelsea katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini alikuwa mwenye furaha kupita kiasi wakati anawapungia mkono mashabiki wa timu hiyo baada ya mechi ya jana.
  Inafahamika mshambuliaji huyo ni chaguo la kwanza la kocha Jose Mourinho katika orodha ya wachezaji anaotaka kuwasajili msimu ujao na kitendo cha kuwapungia kwa furaha mashabiki wa Chelsea jana kimezidi kuongeza dalili za kuhamia kwake London.
  Chelsea ilitoka sare ya bila kufungana na Atletico Madrid Uwanja wa Vicente Calderon, inamaanisha mchezo bado upo kati kwa kati kuelekea mechi ya marudiano Jumatano ijayo.

  Anawapa dalili? Diego Costa akiwapungia mkono mashabiki wa Chelsea baada ya mechi usiku wa jana
  Rivals: The striker could be a team-mate of John Terry's next season, not an adversary
  Upinzani: Mshambuliaji huyo anaweza kuja kuwa mchezaji mwenzake John Terry msimu ujao, japokuwa jana walizinguana sana uwanjani

  Baada ya filimbi ya mwisho mashabiki wa Chelsea walibaki uwanjani wakati baadhi ya wachezaji wanapita mbele yao kuondoka.
  Na wakati Costa alipofika kwenye eneo lao, mashabiki wa Chelsea wakaanza kuimba: "Diego Costa, tutakuona mwaka ujao,".
  Mshambuliaji huyo wa Atletico aliwapigia makofi pia na kuufurahia wimbo huo. Wakati ukifika utatoa majibu katika kipindi cha pili cha Mourinho kuiongoza The Blues na hata kuhusu mustakabali wa mchezaji ghali wa klabu hiyo, Fernando Torres kama rekodi yake itavunjwa?
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DIEGO COSTA AWAPA ISHARA NZURI CHELSEA...NI DALILI ZA KUHAMIA DARAJANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top