• HABARI MPYA

  Jumapili, Aprili 27, 2014

  AHLY YATINGA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO ‘KIZALIZALI’

  Na Mwandishi Wetu, Morocco
  VIGOGO wa Misri, Al Ahly wamefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa bao la dakika za lala salama la Ahmed Raouf.
  Wawakilishi wa Morocco, Difaa Hassani El Jadida walikuwa kwenye nafasi ya kusonga mbele baada ya mabao ya kipindi cha pili ya Ahmed Chagou na mchezaji kutoka Gabon, Johan Lengoualama, kabla ya Raouf kufunga dakika ya mwisho na kuivusha Ahly.

  Kwa matokeo hayo, Ahly inasonga mbele kwa faida ya bao la ugenini kufuatia awali kushinda 1-0 nyumbani hivyo kufanya sare ya jumla ya 2-2.
  Katika mechi nyingine za jana, Bayelsa Utd ya Nigeria ilifungwa 1-0 nyumbani na Sewe Sport ya Ivory Coast na kutolewa kwa jumla ya mabao 2-0.
  Mechi nyingine zinachezwa leo, AS Real na Djoliba zote za Mali, AC Leopards ya Kongo na Medeama ya Ghana, Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Coton Sport ya Cameroon na Petro Atletico ya Angola, Horoya ya Guinea na Etoile du Sahel ya Tunisia na Nkana FC ya Zambia na Club Athletique Bizertin ya Tunisia
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AHLY YATINGA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO ‘KIZALIZALI’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top