• HABARI MPYA

  Jumatatu, Aprili 21, 2014

  MESSI AREJESHA FURAHA BARCELONA, YASHINDA 2-1 LA LIGA

  NYOTA Lionel Messi amehitimisha dakika 348 za kucheza bila kufunga bao, akiiwezesha Barcelona kushinda mabao 2-1 dhidi ya Athletic Bilbao katika La Liga.
  Muargentina huyo alifunga kwa mpira wa adhabu dakika mbili baada ya Pedro had kusawazisha dhidi ya Athletic Bilbao Uwanja wa Nou Camp. 
  Messi aliyecheza mechi tatu bila kufunga, usiku wa jana alifunga bao lake dakika ya 74 wakati Pedro alifunga dakika ya 72 baada ya wageni kutangulia kupata bao dakika ya 50 kupitia kwa Aduriz.
  Barcelona imefikisha pointi 81 baada ya kucheza mechi 34 na inarudi nafasi ya pili, nyuma  ya Atletico Madrid yenye pointi 85 za mechi 34 pia, wakati Real Madrid ina pointi 79 za mechi 33 na Jumamosi itacheza  na Osasuna.  
  Mshindi: Lionel Messi akishangilia baada ya bao lake la ushindi aliloifungia Barcelona usiku wa jana 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MESSI AREJESHA FURAHA BARCELONA, YASHINDA 2-1 LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top