• HABARI MPYA

  Jumapili, Aprili 27, 2014

  STARS KUANZA NA ZIMBABWE KUFUZU MATAIFA YA AFRIKA 2015

  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
  TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imepangiwa kucheza na Zimbabwe katika raundi ya pili ya mechi za mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
  Stars itaanzia nyumbani ambapo mechi ya kwanza itachezwa kati ya Mei 16 na 18 wakati ile ya marudiano itachezwa Harare kati ya Mei 30 na Juni 1 mwaka huu.
  Zimbabwe mzee; Kocha mpya wa Stars, Mart Nooij

  Huu ni mtihani mwingine mgumu kwa Stars, ambayo imefuzu mara moja tu fainali hizo mwaka 1980 nchini Nigeria, kwani mara nyingi Tanzania haina huwa ubavu wa kufurukuta mbele ya timu za Kusini mwa Afrika. 
  Lakini katika kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia mwaka huu Brazil, Stars ikiwa chini ya kocha Mdenmark, Kim Poulsen Stars ilionyesha ukomavu hadi kufikia kuifumua Morocco mabao 3-1 Machi 24 mwaka jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na katika mchezo wa marudiano Juni 8 mwaka huo ikafungwa 2-1 mjini Marakech.
  Kim Poulsen ameondolewa na Stars ipo chini ya Mholanzi, Mart Nooij aliyetambulishwa rasmi jana saa chache baada ya kutua nchini akitokea Ethiopia alikokuwa anaifundisha klabu ya St George.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: STARS KUANZA NA ZIMBABWE KUFUZU MATAIFA YA AFRIKA 2015 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top