• HABARI MPYA

    Thursday, April 17, 2014

    LIGI YA MABINGWA WA MIKOA KUANZA MEI 10

    Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
    LIGI ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) itakayochezwa kwa ligi ya mkondo mmoja katika vituo vitatu vya timu tisa kila kimoja inatarajia kuanza Mei 10 mwaka huu.
    Timu ya kwanza kutoka katika kila kituo ndiyo itakayopanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2014/2015. Kwa vile ligi hii haina mdhamini, hivyo timu zitajigharamia kwa kila kitu.

    Vituo vitakavyotumika kwa ajili ya RCL, kanuni pamoja na ratiba vitatangazwa kabla ya kuanza kwa ligi hiyo. Pia kituo kitakachoteuliwa kwa ajili ya ligi hiyo, timu yake haitapangwa katika kituo husika ikiwa ni moja ya njia ya kuhakikisha kanuni ya mchezo wa kiungwana (fair play) inazingatiwa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIGI YA MABINGWA WA MIKOA KUANZA MEI 10 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top