• HABARI MPYA

  Jumapili, Aprili 27, 2014

  KADO ‘AITALIKI’ COASTAL, AJIPIGA MNADA

  Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
  KIPA Shaaban Hassan Kado amesema hataongeza Mkataba Coastal Union ya Tanga baada ya kumalizika wa awali na anafungua milango kwa timu nyingine zinazomuhitaji kufanya naye mazungumzo.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana mjini Dar es Salaam, Kado amesema kwamba hataki kusema mengi kuhusu Coastal, ila anashukuru kwa misimu miwili aliyokuwa na timu hiyo na anaachana nayo.
  Mimi na Coastal basi; Shaaban Kado amesema hataongeza mkataba na timu ya Tanga na anafungua milango kwa timu nyingine zitakazomtaka

  Jambo zuri kwa Kado ni kwamba anatarajia kufungua plasta gumu (PoP) Mei 5 katika mkono wake wa kushoto na moja kwa moja kuanza mazoezi.
  Kado aliumia katika mchezo dhidi ya Ashanti United Machi mwaka huu na mbaya zaidi akatelekezwa na uongozi wa Coastal hivyo kulazimika kujitibu kwa gharama zake mwenyewe.
  Kipa huyo wa zamani wa Moro United, Mtibwa Sugar zote za Morogoro na Yanga SC ya Dar es Salaam, amesema timu yoyote inayomuhitaji imsake kwa mazungumzo.
  “Nasema mimi kwa sasa ni mchezaji huru na ninaendelea na mazoezi kwa sababu niliumia kiganja cha mkono, ila mazoezi ya kudaka nitaanza kuanzia Mei 10,”alisema Kado ambaye amechezea timu ya taifa, Taifa Stars pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KADO ‘AITALIKI’ COASTAL, AJIPIGA MNADA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top