• HABARI MPYA

  Jumamosi, Aprili 19, 2014

  SIMBA NA YANGA 1-1 TAIFA, AZAM YAILAZA JKT RUVU 1-0 CHAMAZI

  Na Waandishi Wetu, Dar es Salaam
  BAO la Simon Msuva dakika ya 86, jioni hii limeinusuru Yanga SC kulala mbele ya mahasimu wake, Simba SC baada ya kupata sare ya 1-1 katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wakati Uwanja wa Azam Complex, Chamazi bao la Brian Umony limeipa Azam ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Ruvu.
  Himid Mao akiwatoka wachezaji wa JKT Ruvu leo Chamazi
  Simba SC ilitangulia kupata bao kupitia kwa Haroun Chanongo dakika ya 68 na kwa matokeo hayo, Azam inamaliza Ligi Kuu na pointi 62 wakati Yanga SC inamaliza na pointi 56 katika nafasi ya pili- kwa maana hiyo Azam FC ni mabingwa wasiopingika wa Ligi Kuu  2013/2014. HABARI ZAIDI ITAFUATIA. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA NA YANGA 1-1 TAIFA, AZAM YAILAZA JKT RUVU 1-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top