• HABARI MPYA

  Jumatatu, Aprili 21, 2014

  AL AHLY YANUSA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

  TIMU ya Al Ahly ya Misri imebisha hodi hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Difaa El- Jadidi ya Moroco Uwanja wa Jeshi la Anga mjini Cairo Misri jana.
  Shukrani kwake Abdallah Said aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 20 na sasa Al Ahly iliyovuliwa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika itahitaji sare katika mchezo wa marudiano kutinga hatua ya makundi.

  Katika mechi nyingine za jana, AS Real iliifunga 2-1 Djoliba FC zote za Mali, AC Leopards ya Kongo iliifunga 2-0 Medeama ya Ghana, Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini ilifungwa 2-1 nyumbani na ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Coton Sport ya Cameroon ilishinda 2-1 dhidi ya Petro Atletico ya Angola, Horoya ya Guinea ililazimishwa sare ya 0-0 na Etoile du Sahel ya Tunisia, Sewe Sport ya Ivory Coast ilishinda 2-0 dhidi ya Bayelsa Utd ya Nigeria na juzi Nkana ya Zambia ililazimishwa sare ya 0-0 na CA Bizertin ya Tunisia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AL AHLY YANUSA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top